Mikopo ya sekta ya madini
Sekta ya madini ni moja kati ya sekta zinazoongoza nchini; thamani ya mauzo ya nje ya madini imekua ikiongezeka kwa kiwango cha juu kila mwaka. Sekta hii ni muhimu sana kwa uchumi wa taifa kwa kuwa ni chanzo kikubwa cha fedha za kigeni. Shughuli za uchimbaji wa madini zimejikita zaidi kwenye uchimbaji wa madini ya dhahabu, madini ya vito na madini ya viwandani kama kaolini, makaa ya mawe na kokoto.
Mikopo ya sekta ya madini inalenga wakopaji wanaojishughulisha na uchimbaji na uchakataji wa madini kwa ajili ya kuongezea thamani.
Vigezo vya mkopo
- Mikopo hii hutolewa kwa miradi mipya/inayoanza na inayoendelea yenye uhitaji wa maboresho mbalimbali ikiwemo ya miundombinu au mitambo.
- Mikopo hii ni ya muda wa kati na muda mrefu.
- Kutolewa kwa kipindi cha rehema (grace period) wakati wa maandalizi/ujenzi wa mradi
- Riba nafuu kutegemeana na mradi
- Ili kuepuka changamoto za mabadiliko ya thamani ya fedha za kigeni mikopo hutolewa kulingana na fedha ya mapato ya mradi
- Mikopo itatolewa ndani ya muda mfupi baada ya maombi kuwasilishwa
Faida za mkopo
- Kuwezesha wateja kuanzisha miradi kuanzia kujenga miundombinu, ununuzi wa vifaa na mitambo pamoja na usimikaji wake
- Uanzishwaji wa miradi mipya ambayo hapo awali ilionekana kama miradi isiyo na ushawishi wa kibenki
- Ushauri wa kifundi kutoka kwa wataalamu wa benki ili kupunguza mapungufu ya kiufundi katika mradi.