Karibu Benki ya Maendeleo TIB

Mikopo ya Huduma za Nishati na Maji

Tanzania ina rasilimali nyingi za asili na anuwai ambazo bado hazijaendelezwa kikamilifu. Rasilimali za maji na nishati, vyanzo vyake ni pamoja na mito, maziwa kwa upande wa nishati vyanzo vyake ni pamoja na mafuta, miti, umeme unaotokana na maji, gesi asilia, makaa ya mawe, urani, upepo, jotoardhi na jua.

Mikopo hii inatolewa kwa wakopaji kutoka kampuni binafsi na za umma zinazoji shughulisha na utoaji wa huduma za msingi, kama umeme, maji, huduma za maji taka na gesi asilia.

Mikopo ya huduma za nishati na maji zinalenga uwekezaji katika maeneo yafuatayo:

 • Uzalishaji wa nishati, usafirishaji na usambazaji
 • Huduma za maji na maji taka

Sifa za mkopo

 • Kugharamia miradi mipya na inayoendelea ya nishati na maji
 • Ulipaji unaoendana na mapato yapatikanayo katika mradi
 • Kipindi cha rehema (grace period) wakati wa uanzishwaji wa mradi  (ujenzi, uagizaji na usimikaji wa mitambo n.k)
 • Riba nafuu
 • Mkopo kupatikana kwa wakati.

Faida za mkopo

 • Kuwawezesha wateja kushiriki katika miradi ya huduma za nishati na maji
 • Kuziwezesha kampuni kuwekeza bila vikwazo
 • Kuwaunganisha wateja na wawekezaji ili kuwapatia washirika wa kibiashara
 • Kutoa msaada wa kitaalamu ili kuhakikisha ufanisi katika mradi.

Mikopo ya Huduma za Nishati na Maji

blog