Mikopo ya Sekta ya Huduma
Ushiriki wa Benki ya Maendeleo TIB katika sekta ya huduma unalenga maeneo yafuatayo:
- Utalii
- Majengo ya biashara (Commercial Real Estate)
- Sanaa na utamaduni
- Afya
- Elimu
Sifa za mkopo
- Mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kuchachusha maendeleo ya sekta ya huduma; mikopo hutolewa kwa miradi mipya inayoanza na ile inayoendelea.
- Mikopo kwa ajili ya mtaji wa uwekezaji inajumuisha (i.e. ujenzi wa majengo ya biashara, ununuzi wa samani).
- Kipindi cha rehema (Grace period) hii hutolewa kulingana na aina ya mradi.
- Mikopo hii ni ya kipindi cha muda mrefu wa marejesho unaofikia mpaka miaka ishirini (20).
- Mkopaji atachangia kiasi cha 40% ya gharama za mradi.
- Mikopo hii ni ya riba nafuu.
Faida za mkopo
- Marejesho yatategemea na msimu, aina ya uwekezaji na mapato.
- Inawezesha taasisi za umma kufikia malengo ya mradi kwa haraka.
- Inasaidia sekta za umma kuwekeza katika upanuzi wa miradi na uanzishaji wa miradi mpya
- Kuhamasisha maendeleo ya biashara na uchumi ili kuongeza tija kwa maendeleo ya Kitaifa.
- Hupatikanaji wa ushauri wa kitaalamu wakati wa maandalizi ya mradi kwa taasisi za umma.