Mikopo ya Sekta ya Kilimo
1. HUDUMA
Mikopo chini ya dirisha la kilimo itatolewa kuwezesha shughuli za uzalishaji, usindikaji mazao na masoko (kwa wakopaji wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo). Mikopo itakuwa ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kwa kutumia fedha zilizotolewa na serikali. Shughuli za kilimo zitahusisha uzalishaji mazao na ufugaji.
2. WALENGWA
Walengwa katika program hii ni waombaji wote wenye miradi ya kilimo na ufugaji ambao wanauzoefu na wanajihusisha na kilimo, wana historia nzuri ya kilimo na wana uongozi na usimamizi mzuri.
Walengwa halisi katika mpango wa mikopo hii ya kilimo ni pamoja na:
i) Wakulima wadogowadogo na wa kati waliojiunga katika vyama vilivyosajiliwa na mamlaka husika kama vile Ushirika, na vikundi (out-growers of larger farms).
ii) Wakulima wa kati na wakubwa wanaoendesha kilimo cha kibiashara kupitia makampuni. Uainishaji wa mikopo midogo, ya kati na mikubwa utazingatia Sera ya Taifa ya SME.
iii) Taasisi za kifedha zinazo jihusisha na kilimo kama vile Benki Jamii, SACCOS, NGOs, Benki vijiji/VICOBA.
iv) Shughuli za kilimo za kati zinazoongeza thamani kama vile uhifadhi, usindikaji na masoko.
3. GHARAMA
1.1 Riba
Riba itatozwa kwa kiwango cha asilimia tano (5%) kwa mwaka kwa wakopaji wa moja kwa moja toka benki (direct borrowers). Taasisi zinazokopa kwaajili ya kukopesha (on-lenders) zitatozwa asilimia 4 kwa mwaka ambapo zitatakiwa kukopesha kwa asilimia isiyozidi nane (8%) kwa wakulima/wateja wao. Viwango vya riba vinaweza kubadilika itakapobidi.
1.2 Ada za kibenki (bank charges)
Ada zote zinazohusiana na mkopo ikiwa ni pamoja na gharama za ushuru wa stampu, usajiri wa hati za dhamana, mikataba na huduma mbalimbali zikiwemo za kisheria zitalipiwa na mkopaji. Kwa taasisi za kifedha (on-lenders), ada zote za mkopo wa kilimo zitakazotozwa kwa mkulima (final borrower) zinatakiwa zisizidi asilimia mbili (2%).
4. MUDA WA MAREJESHO
4.1 Kipindi cha marejesho
Muda wa kurejesha mkopo utakuwa kati ya miezi sita (6) hadi miaka kumi na tano (15) kwa kutegemea aina ya mradi wa kilimo pamoja na makadirio ya hesabu (financial projections).
4.2 Kipindi cha rehema
Kipindi cha rehema (grace period) kitatolewa kulingana na kipindi cha kukomaa kwa mazao husika pamoja na makadirio ya mtiririko wa fedha (projected cash flow). Kipindi cha juu cha rehema kitakuwa miaka 3 kwa mazao ya muda mrefu na mwaka mmoja kwa mazao ya muda mfupi. Katika kipindi hicho mkopaji atatakiwa kulipia riba ya mkopo ingawa malipo yatazingatia msimu wa mapato.
5. MASHARTI YA MKOPO
Mchakato wa ukopaji, usimamizi na taratibu za kukusanya marejesho;
1) Mwombaji atatuma maombi chini ya mikopo ya Dirisha la kilimo akionyesha aina ya mradi wa kilimo anaotaka kuufanya pamoja na kukamilisha mahitaji mengine.
2) Benki itatathmini maombi hayo na kutambua miradi mizuri au yenye tija, ikionekana inafaa maofisa wa benki watatembelea mradi ulipo (project site visit). Kutembelea mradi kutaisaidia benki kufanya tathmini ya awali ya ubora wa mradi na kujiridhisha kufaa au kutofaa kwa mradi. Endapo mradi utaonekana haufai, mkopaji atajulishwa ipasavyo na hatua za maombi zitasimamishwa.
3) Maombi ya mikopo yatashughulikiwa ndani ya siku 21 za kazi baada ya kupokea maombi yaliyokamilika ambapo mkopaji atatakiwa kupewa jibu mahususi juu ya maombi yake.
4) Benki itazingatia vipindi na misimu ya uzalishaji na mapato katika kupanga marejesho.
5) Katika kutathmini dhamana, mali zitakazotumika kama dhamana ya mkopo, thamani yake itapunguzwa kwa asilimia 20 ili kuzingatia mabadiliko ya thamani katika masoko, kupungua kwa thamani ya mali na bei ya kuuzia katika muda ujao.
6) Mkopaji atatakiwa kuchangia mtaji kwa asilimia 30 ya gharama zote za mradi ambapo kati ya hizo asilimia 10 lazima iwe fedha tasilimu.
7) Kwa majengo kutumika kama mchango wa mkopaji ni lazima (i) yawe na hati miliki ambayo hajiwekwa rehani (ii) Lazima iwe inatumika katika uzalishaji wa mradi husika.
8) Mali itakayotumika kama dhamana ni lazima iwe inamilikiwa na mradi au mkopaji. Dhamana ya mtu wa tatu itatumika tu kama nyongeza.
9) Kufuatia kuidhinishwa mkopo, barua ya ufahamisho itatolewa kwa mkopaji.
10) Fedha zitatolewa endapo dhamana zitakuwa zimesajiliwa na mamlaka husika na baada ya kutimiza masharti ya awali kama yatakavyoainishwa katika barua ya kukubaliwa kwa mkopo. Fedha zitatolewa kulipia vifaa/zana moja kwa moja.
11) Baada ya fedha kutolewa, benki itafanya usimamizi wa karibu wa mradi.
12) Marejesho yatafanywa kama itakavyokuwa imeelekezwa kwenye mkataba. Mpango wa marejesho utazingatia uzalishaji katika mradi.
13) Fedha zitakazotolewa zinakusudia kugharimia uzalishaji, usindikaji mazao na shughuli za masoko.
6. MASHARTI HUSIKA KWA WAKOPAJI
6.1 Taasisi zinazokopesha (On – lenders)
i) Mkopaji ni lazima awe kikundi au taasisi inayotambulika kisheria na imesajiliwa kama vile Ushirika, SACCOS, Benki jamii, Vyama vya Ushirika na Vikundi.
ii) Mkopaji lazima awe na historia nzuri.
iii) Dhamana chini ya fungu hili zitakuwa “outstanding portfolio, fixed deposits and legal mortgage” itakapobidi.
iv) SACCOS na vyama ushirika lazima viwe na cheti cha ukomo wa madeni kutoka kwa msajili wa ushirika.
v) Dahamana zinazoazimiwa na wakopaji kutoka Taasisi ndogo ndogo za kifedha zitachukuliwa na benki (deed of assignment).
vi) Riba itatozwa kwa asilimia nne (4%) kwa mwaka na mkulima wa mwisho chini ya utaratibu huu atakopeshwa kwa kiwaango kisichozidi asilimia 8 kwa mwaka.
vii) Muda wa mkopo na marejesho utakuwa kati ya miezi 6 hadi miaka 15.
xiii) Kiwango cha mkopo kitakuwa kati ya shilingi milioni 50 na shilingi milioni 1,000.
6.2 Wakopaji wa moja kwa moja (Direct borrowers commercial farmers)
i. Mkopaji lazima iwe ni kampuni inayofanya kilimo cha biashara ambayo imesajiliwa
ii) Mkopaji lazima awe na historia nzuri ya uzalishaji.
iii) Dhamana chini ya kundi hili zitakuwa “fixed deposits, debenture, stocks in warehouses, legal mortgage and chattels mortgage”.
iv) Miradi yenye mipango mizuri ya umwagiliaji itakuwa na nafasi kubwa zaidi.
v.) Wakulima wakubwa watakaosaidia wakulima wadogo (out-growers) watakuwa na nafasi zaidi.
vi) Riba itatozwa kwa kiwango cha asilimia 5 kwa mwaka.
vii) Muda wa marejesho utakuwa kati ya miezi 6 hadi miaka 15.
viii) Kiwango cha mkopo kitakuwa kati ya shilingi milioni 50 na shilingi milioni 1,000.
7. DHAMANA (SECURITY STRUCTURE)
Mpango wa dhamana ufuatao utazingatiwa:
i) Mikopo chini ya Dirisha la kilimo itadhaminiwa na ‘debenture’ na ‘mortgage over landed property’, pamoja na machine/zana za kilimo, mazao ghalani, machine za kusindika vyakula, magari, pamoja na mikopo kwa taasisi za kifedha (credit portfolio).
ii) Ikiwa shamba halina umiliki unaotambuliwa kisheria, mali yoyote nyingine isiyohamishika inaweza kutumika kama dhamana ya msingi ilimradi inamilikiwa na mradi husika au mkopaji. Mali isiyomilikiwa na mkopaji haitatumika kama dhamana ya msingi.
iii) Zana au mashine zitakazonunuliwa kupitia Dirisha la kilimo zitachukuliwa kama sehemu ya dhamana baada ya kupunguza asilimia 20 (discount by 20%).
iv) Pale itakapowezekana dhamana lazima zikatiwe bima dhidi ya moto,
v) Endapo mkopo utatolewa kwa kuzingatia mazao katika maghala, usimamizi madhubuti utahitajika chini ya ‘collateral management’. Mkopaji atatakiwa kulipia gharama za ‘collateral management’.
vi) Kiwango cha chini cha thamani ya mali itakayotumika kama dhamana kitakuwa asilimia 125 ya kiwango cha mkopo (hili ni takwa la kisheria - regulatory equirement).
Gharama za usajili wa mikataba ya kisheria italipwa na mkopaji.
MAHITAJI | |
---|---|
VIGEZO VYA UBORA | |
1. Uzoefu katika biashara/shughuli za kilimo (**start ups that meet other critical criteria shall be considered) | mwaka 1 |
2. Upatikanaji na uwepo wa umwagiliaji | Chanya** |
3. Uwezo na uzoefu wa uongozi | Chanya** |
4. Taarifa za hali ya hewa na udongo | Chanya** |
5. Uwepo wa njia za kuzuia wadudu na magonjwa ya mazao | Chanya** |
6. Kuzingatia uhifadhi wa mazingira | Chanya** |
7. Uwepo wa maghala ya kutosha na yanayofaa kwa mazao. | Chanya** |
8. Upatikanaji na uwepo wa masoko | Chanya** |
9. Taarifa za biashara na bei (mwenendo wa bei na biashara) | Chanya** |
MAHITAJI | |
---|---|
VIGEZO VYA UPIMAJI | |
1. Mali halisi/dhima (Net worth) ya mwaka wa fedha uliopita | Chanya** |
2. Mtiririko halisi kutoka shughuli za uendeshaji kabla ya ya riba na kodi | Chanya** |
3. Muda wa juu wa marejesho (Maximum Tenure) | Miaka 15 |
4. Kiwango cha chini cha kukopa kwa mkopaji mmoja | Sh. milioni 50 |
5. Kiwango cha juu cha kukopa kwa mkopaji mmoja | Sh. milioni 1,000 |
6. Kiwango cha mkopo kama asilimia ya gharama zote za mradi | 70% |
7. Kiwango cha chini cha mchango wa mkopaji | 30%** |
8. Kiwango cha fedha tasilimu mchango wa mkopaji | 10%** |
MAHITAJI |
---|
DHAMANA |
Ya lazima (mandatory): a) Hati ya dhamana ya mali zote za kampuni (Debenture on all assets) b) Amana/ rehani ya kwanza ya kisheria kwa shamba / mali ya kibiashara (First priority legal mortgage on farm/business property being financed). c) Mauzo (assignment of receivables from sales). d) Bima ya mali isiyohamishika (fixed & floating assets). e) Mashine, vifaa/zana, n.k. zilizonunuliwa na mkopo |